Ufugaji wa Nguruwe ni kati ya shughuli zinazokua haraka katika Afrika Mashariki na ya Kusini. Ukuaji wa miji na ongezeko la watu kumeendana...
Nyumba ya nguruwe
Kwa ujumla nyumba za aina mbili huhitajika katika ufugaji wa nguruwe
1.Nyumba za kukuzia na kunenepesha nguruwe wa kuchinja
2. Nyumba za nguruwe wazazi
Sifa za msingi za nyumba bora ya nguruwe
• Nyumba ijengwe eneo lenye kivuli cha kutosha
• Nyumba iwe na nafasi ya kutosha
• Ijengwe sehemu yen ye mwinuko kiasi ili kuwezesha maji
kuondoka kwa urahisi
• Iwe na chombo/kihori cha kuweka chakula na kingine chakuweka
maji
• Iwe na sakafu imara iliyotengenezwa kwa saruji, mabanzi,
miti na isiwe na unyevu
• Sakafu ya saruji iwe na mteremko (slope) inayoweza kuondoa
uchafu kwa urahisi
ndani ya banda.
• Sakafu ya mabanzi, mbao au miti iwe inatoa nafasi ya
kuondoa uchafu kama kinyesi
ndani ya banda.
• Iwe na mtaro wa kuondolea maji, mkojo na kinyesi hadi
shimo la kutunzia
• Kuta za mabanda ya nguruwe zinatakiwa kuwa imara, ziwe na
uwezo wa kuwasitiri
nguruwe wasitoke nje
• Iweze kuingiza hewa ya kutosha ndani ya banda hasa kama
ukuta umezibwa (solid walls)
Upate wapi Nguruwe wa Kufuga
Nunua nguruwe wa kufuga kutoka kwenye mashamba au wafugaji
wanaoaminika ukizingatia
yafuatayo.
• Usizalishe nguruwe wanaotokana na ukoo mmoja yaani ndugu
kama kaka ria dada.
Nunua dume na jike toka mahali tofauti.
• Tumia ushauri wa wataalamu kuchagua nguruwe bora
Sifa za kuangalia kwa nguruwe bora wa mbegu
• Nguruwe wa mbegu awe na sifa ya kukua haraka na asiwe na
ulemavu wa aina yeyote, na
hasa wa miguu kwa dume.
Mama mzazi wa nguruwe awe na historia ya kuzaa watoto 10
hadi 12 kwa mzao mmoja
• Jike awe na chuchu zaidi ya 12.
• Dume awe na sehemu za kiume yaani korodani na uume
unaoonekana sawa sawa. Pia awe
na hamu ya kupanda majike.
Mbinu za uzalishaji
Matunzo ya dume la uzalishaji
• Chagua dume la mbegu bora, lisilokuwa na kilema au ugonjwa wowote.Tenganisha dume na majike ili kuepusha kupandwa kusiko na kumbukumbu. Dume la nguruwe halipaswi kunenepa, kwa hiyo usimlishe chakula kingi na mpatie mazoezi ya kutosha asije akawa mvivu
• Nguruwe dume anaanza kupanda majike akiwa na umri wa miezi 4 hadi miezi 9. Dume liruhusiwe kupanda mara moja tu kwa kila juma. Anapofika miezi 10 anaweza kupanda mara mbili hadi mara tatu kwa wiki. Akiwa na mwaka mmoja na zaidi anaweza kupanda kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa majuma mawili. Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande majike 15 hadi 20 kwa mwaka.
• Madume madogo yapande majike madogo, dume kubwa likimpanda jike dogo anaweza akamletea maradhi ya mgongo. Ni muhimu kupandisha dume kabla hajala chakula, na asitumiwe mara tu baada ya chakula iii asiwe mvivu
Utunzaji nguruwe mwenye mimba
• Mimba ya nguruwe huchukuwa miezi mitatu (3) wiki tatu(3)
na siku tatu(3) yaani siku 114
• Nguruwe mwenye mimba apewe chakula cha kutosha kiongezwe
polepole tokea posho ya kawaida hadi kilo 3 - 3. 5 kwa siku
Matayarisho ya nyumba kabla ya kuzaa
• Osha banda la kuzalia kwa maji na kuliacha likauke
• Tandika nyasi kavu mara baada ya nyumba kukauka
• Ongeza taa ya chemli au umeme kama uko mikoa yenye baridi
kwenye sehemu ya vitoto.
• Tengeneza sehemu ya kuzalia kwa mbao au mabomba
• Mpe dawa ya rninyoo siku 10 kabla ya kuzaa
• Mogeshe mama nguruwe kwa sabuni ya mkono na brashi
• Muhamishie katika chumba cha kuzalia siku 7 kabla hajazaa
• Mpunguzie lishe siku 2 kabla ya kuzaa
• Siku ya kuzaa mpe nguruwe maji ya kunywa tu
Upandishaji jike
• Kati ya siku nne hadi saba baada ya kuachishwa watoto,
nguruwe mama hupata joto.
Nguruwe jike alie kwenye joto apelekwe kwenye banda la dume
na sio kinyume chake. Rudia
kumpandishajike alie kwenye joto masaa 12 baada ya mpando wa
kwanza; rudia
kumpandisha mara 2 hadi 4. Kamajike hatarudia kwenye joto
baada ya wiki 3 atakuwa
ameshika mimba
Dalili za joto
• Sehemu ya uzazi kubadilika na kuwa nyekundu
• Nguruwe hatulii na hukojoa mara kwa mara
• Ute kama makamasi hutoka sehemu za siri
• Nguruwe mwenye joto hujaribu kuwapanda wenzake na yeye
akipandwa hutulia
UTUNZAJI WA VITOTO VYA NGURUWE
Ulishaji wa maziwa ya kwanza
Baada ya kuzaliwa na kusafishwa, hakikisha vitoto
vinanyonyeshwa. Vitovu viwekewe dawa (Iodine
5%) iii kuzuia magonjwa. Kama mama amefariki mara tu baada
ya kuzaa na hakuna nguruwe
mwingine anayeweza kunyonyesha; tumia maziwa ya ng'ombe.
ongeza sukari na yai bichi koroga na
uwanyonyeshe kwa kutumia chupa ya maziwa ya mtoto.
Joto
Vitoto vya nguruwe havizaliwi na manyoya na hawana mafuta
mengi ya kutosha kuwaletea joto
mwilini; hivyo ni rahisi kufa kwa baridi. Tumia taa ya stimu
au chemli kuongeza joto.
Kuzuia upungufu wa damu
Maziwa ya nguruwe yana upungufu wa madini ya chuma
yaongezayo damu. Hivyo baada ya
majuma mawili au matatu watoto huanza kudhoofu kwa kukosa
madini hayo mwilini. Kuondoa
tatizo hili inabidi vitoto vidungwe sindano ya madini kwenye
misuli siku mbili au tatu tangu
kuzaliwa. Kama sindano haipatikani njia nyingine za
kuwapatia watoto madini hayo ni kwa kuwapa
vidonge vya madini chuma, au kuwapa madini hayo kwen_ e
ndimi zao au chuchu za mama yao siku
mbila hadi tatu baada ya kuzaliwa
Ukataji meno
Siku chache kabla ya kuzaliwa,meno yaliochongoka kama sindano
huchomoza katika taya mbili.Meno hayo humuumiza mama wakati watoto
wanaponyonya,matokeo yake mama hupiga watoto mateke.Hii husababisha vifo vya
watoto kutokana na kupigwa na kukosa maziwa ya mwanzi hivyo inabidi kupunguza
madhara hayo
Chakula bora kwa nguruwe ni moja ya mahitaji muhimu sana
kwenye dhana nzima ya ufugaji wa
nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha nguruwe
kinagharimu yapata asilimia hamsini
sabini ya gharama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya
matatizo mengi yanayosababisha tija na
ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe
duni. Nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija
na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida
kwa mfugaji.
Kuachisha kunyonyesha
• Viachishe vitoto kunyonya wakifikia umri wa miezi miwili
wanapokuwa na uzito wa kilo 10.
Siku ya kuachisha kunyoyesha muondoe mama nguruwe kwa watoto
wake na kumuweka
chumba kingine
• Mpe mama chakula cha kutosha
Kuhasi
Vitoto ambavyo havihitajiki kwa ajili ya kizazi bora katika
mfugo, vihasiwe vikiwa katika juma la
tatu hadi la nne. Nguruwe walio hasiwa huwa wapole, wenye
nguvu, wazito na nyama yao haina
harufu ya dume. Bwana mifugo atakupa maelezo zaidi
kuhusujinsi ya kufanya.
Baadhi ya faida za lishe bora kwa nguruwe ni:
1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa nguruwe na
hivyo kupata uzito unaohitajika kwa
kipindi kifupi.
2. Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza
faida kwa mfugaji kwa sababu
nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua
muda mfupi kupata uzito mkubwa
3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na
mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi
ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa
na mama nguruwe kwa ajili ya
watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha
wakue haraka na kupunguza
idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na
hivyo kuongeza uwezo wa kupanda
. Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe
Nguruwe wana uwezo wa kula aina nyingi za vyak:ula lakini
vyenye uwezo wa kumeng'enywa kwa
urahisi. Chakula cha nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa
na mchanganyiko wa viini lishe vitano,
navyo ni
1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (kama pumba za
mahindi, ngano, mchele)
2. Vyakula vya kujenga mwili (kama mashudu ya alizeti,
pamba, unga wa dagaa)
3. Vyakula vya asili ya madini (kama chumvi, chokaa, mifupa
iliosagwa)
4. Vyak:ula vya asili ya vitamini (kama majani mabichi,
mbogamboga na matunda)
5. Maji
Baadhi ya faida za lishe bora kwa nguruwe ni:
1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa nguruwe na
hivyo kupata uzito unaohitajika kwa
kipindi kifupi.
2. Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza
faida kwa mfugaji kwa sababu
nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua
muda mfupi kupata uzito mkubwa
3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na
mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi
ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa
na mama nguruwe kwa ajili ya
watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha
wakue haraka na kupunguza
idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na
hivyo kuongeza uwezo wa kupanda
7. Vyakula na ulishaji
Chakula bora kwa nguruwe ni moja ya mahitaji muhimu sana
kwenye dhana nzima ya ufugaji wa
nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha nguruwe
kinagharimu yapata asilimia hamsini
sabini ya gharama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya
matatizo mengi yanayosababisha tija na
ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe
duni. Nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija
na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.
Jinsi ya kutengeneza
chakula cha nguruwe
Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia
yafuatayo:
• Mchanganyiko wake uwe na viinilishe vinne vilivyotajwa
hapo juu
• Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana kwa
urahisi na bei nafuu kwenye mazingira
yako
• Aina ya mchanganyiko wa chakula ni muhimu uzingatie
mahitaji ya nguruwe kama umri (mfano:
nguruwe wanaonyonya, waliochishwa kunyonya, wanaokua, na
wanaonyonyesha)
Kiasi na namna ya kulisha
Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula mara mbili
(asubuhi na mchana) au zaidi kwa
siku
• Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na rika
tofauti kimeonyeshwa kwenye jedwali
Namba3
• Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji wanashauriwa
kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya
kijadi kama vyakula vya ziada mfano, majani mabichi laini,
majani ya maboga, mbogamboga,
matunda kama maparachichi, majani ya viazi n.k
BILA SHAKA UMEPATA KITU
Acha maoni yako hapo chini,AHSANTE
No comments