Magonjwa ya mlipuko sio kitu kigeni yamekuwepo kwa muda mrefu lakini huu ugonjwa wa Corona umekuwa hatarishi kuliko ugonjwa mwingine ule wa ...
Magonjwa ya mlipuko sio kitu kigeni yamekuwepo kwa muda mrefu lakini huu ugonjwa wa Corona umekuwa hatarishi kuliko ugonjwa mwingine ule wa mlipuko uliowahi kuikumba dunia.Dunia imetulia tuli,lugha inayozungumzwa ni moja.Mambo mengi bado yanasemwa sana juu ya ugonjwa huu ila leo katika makala hii tutaangazia filamu na vitabu vilivyotabiri gonjwa hili lililoitikisa dunia.
Kazi za fasihi mbali na kutuburudisha na kutuelimisha ila huwa zinaangazia nadharia mbalimbali ambapo baadhi yake hugeuka kuwa ukweli.Hebu tuanze kwa kuangazia vitabu vitabu na filamu jinsi zilivyotabiri ugonjwa huu wa corona
1. END OF DAYS: Predictions and Prophecies about the end of the world
(SIKU ZA MWISHO: Utabiri na Unabii juu ya mwisho wa dunia)
Kitabu hiki kilichoandikwa na
Sylivia Browne akishirikiana na
Lindsay Harrison na kuchapishwa mwaka 2008 kilitoa utabiri juu ya ugonjwa wa corona,katika moja ya kurasa ya kitabu hicho anaandika
"In around 2020 a severe pneumonia-like illness will spread throughout the globe, attacking the lungs and the bronchial tubes and resisting all known treatments. Almost more baffling than the illness itself will be the fact that it will suddenly vanish as quickly as it arrived, attack again ten years later, and then disappear completely."
Akimaanisha, Mnamo karibu mwaka 2020 ugonjwa mbaya wa pneumonia utaenea ulimwenguni kote, ukishambulia mapafu na mirija ya bronchial na hautakua na dawa ya kuutibu. Utapelekea hali mbaya zaidi kuliko ugonjwa wenyewe na itakuwa kwamba utatoweka ghafla haraka kama ulivyofika, utaendleza maambukizi takribani miaka kumi baadae, na kisha utapotea kabisa.
Kutokana na maneno hayo ni dhahiri kuwa ugonjwa aliouzungumzia ni corona maana ni ugonjwa unaoathiri mapafu kama alivyoandika.Pia katika kitabu hikihiki alitabiri kuwa uchumi wa dunia utashuka na Robot ndo zitakazokuwa zikifanya kazi badala ya watu.Browne alishaaga dunia mwaka 2013
2.THE EYES OF DARKNESS written by Dean Koontz
Riwaya ya The eyes of darkness, iliyoandikwa na Dean Koontz mnamo 1981, ilitaja virusi ambavyo mwandishi aliviita Wuhan-400. Katika riwaya hii, anaelezea jinsi virusi hivyo viliundwa kama silaha katika maabara.
Uhusiano na Covid-19 unakuja kwa kuwa virusi vya corona vilianzia uchina.Japo kitabu hiki hakikutabili moja kwa moja ila uhusiano na Wuhan ambapo ndo kitovu cha Corona unafanya kiwekwe miongoni mwa vitabu vilivyotabiri kuhusu Corona.
3.LES PROPHE´TIES written by Michel
de Nostredame, a.k.a. Nostradamus
Nostradamus ambaye alikuwa Mfaransa mwenye asili ya kiyahudi anaaminika kutabiri matukio mengi ambayo yametokea mpaka sasa kupitia mashairi.Unaweza ukashangaa sana jinsi utabiri wake ulivyofanana na utabiri ambao upo katika riwaya ya coronavirus. Katika kitabu cha ushairi cha Les Prophéties alichokiandika mwaka 1555.Katika kitabu hicho alitabiri juu ya corona,katika kitabu hicho anaandika
"There will be a twin year (2020) from whicch will arise a queen(Corona) who will come from east(China) and who will spread a plague (Virus) in the darkness of night,on a country with 7 hills (Italy) and will transform the twilight of men into dust (death) .to destroy and ruin the world.It will be the end of the world economy as you know it"
Alimaanisha, "Kutakuwa na mwaka pacha (2020) ambao atatokea malkia (Corona) atatoka mashariki (Uchina) na atasambaza janga (Virus) kwenye giza la usiku, kwenye nchi yenye milima 7 (Italia ) na itabadilisha jioni ya wanadamu kuwa vumbi (kifo) na kuharibu ulimwengu.Huo utakuwa mwisho wa uchumi wa dunia kama unavyojua "
4.CONTAGION directed by Steven Soderbergh
Filamu hii iliyoandikwa na Scott Burns na kuongozwa na Steven Soderbergh ina visa vinavyoendana na ugonjwa wa mlipuko wa corona.Katika filamu hii kirus kiitwacho MEV-1 hops kilichotoka kwenye popo na baadae kubainika kwenye nguruwe na hatimae kumfikia binadamu katika mazingira ya huko Hongkong China.
Kutokana na kisa hicho kuna mfanano na virusi vya corona ambapo wanasayansi walivotafiti,walibaini kuwa virusi hivyo vinapatikana kwenye popo.Katika filamu hii ugonjwa huu unaathiri wengi kama Corona.
Asante kwa kusoma. MAKALA IJAYO IHUSU NINI?
Acha maoni yako hapo chini
Kaka makala nzuri Sana nimepata kitu kipya
ReplyDeletetuko pamoja mkuu
Delete