Page Nav

HIDE

Grid

GRID_STYLE

Classic Header

{fbt_classic_header}

Header Ad

//

Breaking News

latest

SOKA : WAFAHAMU WACHEZAJI 5 WENYE MAJINA MAREFU SANA

SOKA : WAFAHAMU WACHEZAJI 5 WENYE MAJINA MAREFU SANA Imekuwa ni kawaida kusikia majina ya wachezaji pindi wanapotangazwa...

SOKA : WAFAHAMU WACHEZAJI 5 WENYE MAJINA MAREFU SANA

Imekuwa ni kawaida kusikia majina ya wachezaji pindi wanapotangazwa kupitia Television au Radio wakati mpira ukichezwa, wengi huwa tunatambua majina ya kawaida na mafupi kutokana na namna ya matamshi ambayo mtangazaji hutamka. Stori kutoka onebiselumedia hii ndio Top 5 ya majina marefu zaidi kwa wachezaji soka, huenda wakawepo wengine ila imenifikia list hii.

Manuel Marouan da Costa Trindade Senoussi:

 ni staa aliyezaliwa Saint Max Ufaransa ambaye jina lake lina jumla ya herufi 36. Kwa sasa anaitumikia klabu ya Olympiacosinayoshiriki Super League ya Ugiriki, amewahi pia kuichezea West Ham Unitedya Uingereza, staa huyu huwa anacheza kama beki wa kati.

Henrique Hilário Meireles Alves Sampaio:

ni mzaliwa kutoka Ureno ambaye amestaafu kucheza soka, alicheza katika nafasi ya Golikipa, amebahatika kucheza kwenye timu yake ya taifa na klabu tofauti ikiwemo Chelsea ya Uingereza. Jina lake lina jumla ya herufi 35.
Fredrik Olof Esaias Stoor Siekkinen:

Anajulikana zaidi kama Fredrick Stoor ambaye amezaliwa Sweden, kwa sasa anaichezea timu ya Viborg FF inayoshiriki Danish Superliga ya Denmark. Stoor anacheza kama beki wa kulia. Ameshawahi kuitumikia klabu ya Fulham ya Uingereza pamoja Derby Country na timu ya taifa ya Sweden. Jina lake lina herufi 31.
Geovanni Deiberson Maurício Gómez:

ni Mbrazil ambaye tayari amestaafu kucheza soka, anatambulika zaidi kwa jina la Geovanni, alikuwa akicheza kama kiungo mshambuliaji akiwa na uwezo wa kucheza pia nafasi ya winga. Geovanni amewahi kuzichezea FC Barcelona, Manchester City, Hull City, Benfica na timu ya taifa yaBrazil. Jina lake lina jumla ya herufi 30.
Diniyar Rinatovich Bilyaletdinov 

 jina ambalo limekuwa likitumika na wengi kumuita, ni mzaliwa kutoka Moscow, Urusi ambaye hivi sasa anaitumikia timu ya Rubin Kazaninayoshiriki Ligi Kuu Urusi. Bilyaletdinov amewahi kucheza katika nafasi ya kiungo akiwa na vilabu vya Locomotive Moscow, Everton na amecheza timu ya taifa ya Urusi. Jina lake lina herufi 30.

3 comments

  1. Kaka hayo majina hayawez kuwa dawa ya corona kwelii!! 😂😂😂

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahah majina marefu kinyama 😝😝😝 ndani yake kuna udawa hahahahah

      Delete