FUGA KIBIASHARA : JINSI YA KUJENGA BANDA LA NGURUWE KITAALAMU Banda la nguruwe huwa halijengwi ilimradi,kuna utaalamu u...
Banda la nguruwe huwa halijengwi ilimradi,kuna
utaalamu unahitajika.Nimekuorodheshea hatua za kufuata pamoja na picha
nimekuwekea ili ujenge banda lako la nguruwe vizuri.SOMA TARATIBU NA KWA
UMAKINI
1. Uchaguzi wa eneo la kujenga banda
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati unapendekeza
eneo la kujenga banda au nyumba
ya nguruwe
i.
Liwe ni eneo lililo kwenye mwinuko japo kidogo
kiasi cha kutotuamisha maji ya
mvua
ii. Ni vizuri eneo likawa na kivuli cha miti ya
asili au kupandwa na liwe na uwezo
wa kupitisha hewa ya kutosha
iii. Ni vizuri likawa mbali kidogo na makazi ya
watu hasa kama unataka kufuga
nguruwe wengi.
iv. Pia kama unataka kufuga nguruwe wengi, ni
vizuri eneo likawa karibu na
barabara au liwe linafikika kwa gari ili iwe
rahisi kusafirisha nguruwe wako
wakati wa kufanya biashara.
2. Mpango wa ujenzi wa banda au nyumba nzuri wa
nguruwe
Mambo ya muhimu kwenye nyumba ya nguruwe ni kama
ifuatavyo;
i.
Sakafu ya nyumba lazima iwe ya mita 3 kwa 3
ii. Sakafu ya nyumba lazima iinuke sentimita 60
juu ya ardhi
iii. Paa lazima liwe na uwezo wa kuzuia mvua kwa
asilimia 100
iv. Upande mmoja wa paa lazima uinuke zaidi ya
mwingine, ule upande mrefu zaidi
utazame mwelekeo usio wa jua ili kukinga mwanga
makli wa jua. Lakini
hakikisha kuwa mwanga wa wa jua unaingia ndani
ya banda na kivuri kipo
upande mmojawapo.
v. Banda au nyumba ijengwe kwa uimara wa
kutosha, lakini ni vizuri kutumia vifaa
vinavyopatikana katika eneo husika kwa bei
rahisi. Banda au nyumba ijengwe
kwa kuzingatia aina ya ufugaji na hali ya hewa
ya mahali husika.
vi. Banda au nyumba ya nguruwe ni vema ikawa
yenye kuleta furaha kwa nguruwe
na si mateso; iwe na hewa nzuri, kivuri cha
kutosha, isiyo na unyevunyevu, joto
kali, harufu mbaya wala matope.
vii. Banda au jingo lijengwe kwa urefu
unaotazama Mashariki-Magharibi ili kukinga
jua na mvua.
viii. Banda au nyumba ya nguruwe igawanywe
katika maeneo madogo madogo
(pens) yatakayoweka nguruwe kulinga na umri wao
wa kuzaliwa. Namba na
idadi na ukubwa wa vyumba utategemea na namba ya
nguruwe inayotarajiwa
kuwekwa au kuzaliwa katika uzazi husika.
ix. Gharama za ujenzi wa banda au nyumba ya
nguruwe zitegemeane sana na
aina ya uzalishaji unaotarajia kuufanya ili
uzalishaji uweze kuwa wenye tija.
3. Aina za sakafu
Kimsingi, kuna aina kuu tatu za sakafu
zinazotumiwa na wafugaji wa nguruwe sehemu
mbalimbali duniani kama inavyoonekana kwenye
picha hapa chini:
4. Mahitaji ya nafasi kwa nguruwe
Mahitaji ya nafasi katika ya nguruwe katika
banda au nyumba ya nguruwe inategemea
na aina ya nguwruwe walioko kwenye nyumba ya
nguruwe.
i. Nguruwe wadogo
Hawa ni nguruwe walioachishwa kunyonya, wana
hitaji mita za eneo la mraba kuanzia
0.3 hadi 0.5 kwa kila kitoto kimoja cha nguruwe.
Hivyo ili kujua ukubwa wa chumba (pen)
cha kukaa vitoto hivyo zidisha hiyo namba na
idadi ya vitoto vya nguruwe unaotaka
kuwaweka.
Picha: Mfano mzuri wa banda la vitoto vya nguruwe lenye nafasi ya kukidhi
mahitaji wa
nguruwe.
-Sakafu ya banda au nyumba ya nguruwe ijengwe
kwa simenti au kwa udongo mgumu
lakini isiwe ya kuteleza. Sakafu pia iwe na
mteremko mdogo kurahisha usafishaji na
maji na kuruhu sakafu kukauka kwa haraka na
isiwe na mibonyeo yeyote.
ii. Nguruwe dume:
Nguruwe dume kwa ajili ya kuzalisha wanahitaji
nafasi ya eneo la mraba kati ya mita 6
Kuja tarehe 8.
-Uangalizi mkubwa kwa nguwe dume unahitajika
maana anaweza kutoka ndani ya
banda na kufuata majike hasa yaliyoko kwenye
joto (majike yaliyotayari kwa kupandwa).
iii. Nguruwe wenye mimba
Nguruwe wenye mimba wanahitaji nafasi kati ya
mita 1.5 hadi 2.0 za eneo la mraba
kwa kila nguruwe mmoja.
Nguruwe wenye mimba wanahitaji mazingira yenye
utulivu sana. Wakati mwingine
nguruwe mwenye mimba anahitaji chumba cha peke
yake. Katika mazingira ya joto ni
vizuri kuweka angalau nguruwe wasiozidi watatu
kwa chumba kimoja.
iv. Nguruwe
wanaonyonyesha
Nguruwe wanaonyonyesha wanahitaji nafasi kati ya
mita 4 hadi 6 za eneo la mraba kwa
kila nguruwe.
Nguruwe wanaonyonyesha pia wanahitaji mazingira tulivu, hivyo wanapaswa wapewe
chumba cha peke yao. Chumba chao kinahitaji kiwe
na vitu vifuatavyo; sehemu ya
kuzalia, vifaa vya kutoa na kupunguza joto,
kiota/chumba cha nguruwe wadogo,
chombo cha chakula cha watoto na chakula cha
mwanzo cha watoto.
Banda la kuzalia
Taa ya kuongeza joto
Chombo cha chakula cha watoto
Kiota/chumba cha watoto
v. Nguruwe wa
Kunenepeshwa
Nguruwe wa kunenepeshwa wanahitaji nafasi kati
ya mita 0.5 hadi 1.0 eneo la mraba
kwa kila nguruwe.
-Sakafu ya banda au nyumba ya nguruwe ijengwe
kwa simenti au kwa udongo mgumu
lakini isiwe ya kuteleza. Sakafu pia iwe na
mteremko mdogo kurahisha usafishaji na
maji na kuruhu sakafu kukauka kwa haraka na
isiwe na mibonyeo yeyote
5. Aina mbalimbali za nyumba na au mabanda ya
nguruwe
Zipo aina mbalimbali za nyumba na au mabanda ya
nguruwe yanayotumika sehemu
mbalimbali duniani na hasa maeneo ya vijijini.
Mifano ya nyumba au mabanda
unazoweza kujenga ni kama inavyoonyesha kwenye
michoro hapa chini:
6. Vyombo vya chakula
Chombo cha chakula lazima kishikiliwe vizuri
kwenye sakafu ili nguruwe
wasikiyumbishe na kumwaga chakula. Ukubwa wa
chombo cha chakula utategemea
sana umri wa nguruwe unaotaka kuanza nao kufuga
au ulio nao. Jedwali hapa chini
kitakusaidia sana kutengeneza chombo
kitakachokidhi mahitaji ya nguruwe wako.
Vyombo vya chakula visafishwe kila siku ili
kuweka chakula safi kitakacho mvutia
nguruwe kula chakula. Na view na umbali wa
kutosha kati ya chombo na chombo
kumruhusu nguruwe kuchagua chakula anachotaka.
7. Vyombo vya maji
Vyombo vinavyotumika kwa chakula vyaweza pia
kutumika kuwekea maji ya
kunywesha nguruwe kama inavyoonekana hapa chini hasa kwa mashamba madogo.
Kwa mashamba makubwa mfumo wa bomba unaweza
kutumika kwa kuingiza
mabomba ya maji ndani ya nyumba ya nguruwe
(automatic drinkers) na nguruwe
wakanywa maji kwa muda wanaotaka wao (tazama
kielelezo hapa chini).
Nguruwe wanahitaji maji safi naya kutosha kwa
siku, na mahitaji yao kulingana na umri
wa nguruwe ni kama yalivyo kwenye jedwali hapa chini.
Maji yanapaswa yawepo muda
wote ili kumruhusu nguruwe kunywa maji kwa kadri
na muda atakao yeye.
KUMBUKA:
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa
(FAO). Kitabu cha Mkulima juu
Uzalishaji wa nguruwe (Kwa wamiliki wadogo
katika kiwango cha kijiji)
JE,UNATAKA SOMO GANI JINGINE,COMMENT HAPO CHINI.
AHSANTE
au nitafute
+255753039599 Whatsapp
No comments