Sabuni ya maji ni rahisi sana kuteng eneza. A nza kute ngeneza hela sasa.Soma kwa umakini,hatua kwa hatua .Fursa ndio hii ndugu yangu hebu ...
Sabuni ya maji ni rahisi sana kutengeneza. Anza kutengeneza hela sasa.Soma kwa umakini,hatua kwa hatua .Fursa ndio hii ndugu yangu hebu ichangamkie na endapo utakuwa na swali lolote lile basi niulize kwenye comment na mimi nitakujibu
1. MAHITAJI
Ø Sulphonic (LABSA)
Ø Slec
Ø Pafyumu (lemon)
Ø Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
Ø Chumvi nzuri ya mawe.
Ø Glycerin
Ø Soda ash light.
Ø Formalin na alka
Ø Maji yaliyokuwa safi
Ø Chombo zaidi ya lita 25.
2. JINSI YA KUTENGENEZA
i.
Chukua
sulphonic moja ujazo wa lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea chenye ujazo wa lita 25
ii.
Kisha
chukua Slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka
iii.
sulphonic
kisha changanya kwa pamoja.
iv.
Chukua
soda ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine
pembeni , kisha chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako
chenye mchanganyiko wa sulphonic na Sles weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10
kuwa makini kwasababu utavimba sana.
v.
Kisha
weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi kutokana na rangi unayoitaka lakini
angalia isizidi sana koroga tena vizuri.
vi.
Kisha
chukua Glycerin vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni
katika chombo chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana.
vii.
Kisha
weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) , hii itafanya sabuni yako
inukie kwa harufu vizuri.
viii.
Koroga
chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai kisha mimina
katika mchanganyiko wako na malizia kiasi cha maji mpaka kufikia lita 25 ambazo
ni wastani kabisa.
ix.
Kisha
weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka formalin kisha
koroga tena vizuri. (alka na formalin sio lazima sana hata kama hautavitumia
sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).
3. ANGALIZO
i.
Chumvi
ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwa sababu hiyo kuwa
makini sana.
ii.
Mchanganyiko
wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa
makini.
iii.
Kuna
baadhi ya malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama MASKI NA
GLOVES.
Nashukuru kaka
ReplyDelete