Rais Dkt. John Pombe Magufuli au JPM ni rais mwenye heshima ya kipekee Afrika na duniani kote kutokana na kuwa na misimamo mikali na hayumb...
Akizungumza kutokea Chato, mkoani Geita wakati wa hafla fupi
ya kumwapisha Waziri wa katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, Rais Magufuli alieleza
wasiwasi wake juu ya mashine hizo huku akitolea mfano jinsi sampuli kutoka
kwenye papai, mbuzi na ndege aina ya kware zilivyotoa majibu kuonesha kwamba
wahusika wana maambukizi ya Corona.
Kauli yake hiyo, imeripotiwa na vyombo vikubwa vya habari
duniani, kuanzia televisheni za BBC, DW, CBS, VOA, AL Jazeera, Sky News, CNN na
kadhalika, huku magazeti ya New York Times, Financial Times, Daily Mail, The
Guardian, Times of India yakiipa uzito habari kuhusu alichokizungumza.
Shirika la Habari la Reuters, nalo pia limeiripoti habari
hiyo kwa ukubwa katika vyombo vyake mbalimbali, na kuzidi kuifanya hotuba ya
Magufuli kuwa mjadala unaoumiza vichwa vya wanasayansi duniani kote kuhusu
ubora na ufanisi wa vifaa vinavyotumika kupima Corona duniani kote.
Vyombo hivyo vya kimataifa, ambavyo mara kwa mara
hushutumiwa kuandika habari mbaya pekee kutoka barani Afrika, safari hii
vimejikuta vikiizungumzia habari ya hotuba ya Rais Magufuli kwa uzuri kwa
sababu alichokibaini kuhusu ufanisi wa mashine hizo, kinahitaji mjadala mpana
wa kitaalamu.
Katika hafla ya kumwapisha Mwigulu, Rais Magufuli alieleza
jinsi sampuli kadhaa zilivyopelekwa kwenye Maabara Kuu ya Taifa, bila ya
wataalamu wa maabara hiyo kujua kuwa si za binadamu, kisha majibu yakatoka
kwamba sampuli hizo zilizokuwa zimepewa majina ya binadamu, zilikuwa na Corona
wakati kiuhalisia zilikuwa ni sampuli za papai, ndege kwale pamoja na mbuzi.
“…Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu
hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza… kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania
msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita...,”
alisema Rais Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla hiyo.
Vyombo hivyo vimeendelea kumnukuu Rais Magufuli akisema:
“…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa
maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa
kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli
zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani
kinafanywa.”
Rais Magufuli, ambaye hadi sasa anatajwa kuwa rais kutoka
nchi za Kiafrika anayeheshimika duniani kote kutokana na kuwa na misimamo
isiyoyumbishwa, alisema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao
walipewa majibu yasiyo sahihi kwamba wameambukizwa Corona wakati si kweli na
kuongeza pengine kuna waliopoteza maisha kwa sababu ya hofu.
Rais Magufuli pia alivishutumu vyombo vya habari vya
kimataifa kwa namna vinavyoripoti kuhusu janga hilo nchini Tanzania licha ya
kuwa vyombo hivyo vipo katika maeneo ambayo yameathirika na ugonjwa huo kuliko
hata Tanzania.
No comments