Page Nav

HIDE

Grid

GRID_STYLE

Classic Header

{fbt_classic_header}

Header Ad

//

Breaking News

latest

CORONAVIRUS (COVID-19): TRUMP, VIRUS VYA CORONA SHAMBULIO HATARI KUWAHI KUIKUMBA MAREKANI,AILAUMU CHINA

Rais wa Marekani, Donald Trump ameelezea  janga la virusi vya corona kama "shambulio baya zaidi" kuwahi kutokea katika taifa hilo...



Rais wa Marekani, Donald Trump ameelezea  janga la virusi vya corona kama "shambulio baya zaidi" kuwahi kutokea katika taifa hilo kubwa duniani, akielekeza kidole huko China.

Bwana Trump alisema kuzuka kwa ugonjwa huo wa Covid-19 kumeathiri sana Marekani kuliko mabomu ya Kijapani yaliyopigwa katika bandari ya Pearl katika Vita vya pili vya dunia, au shambulio la kigaidi  la 9/11 lililotokea miongo miwili iliyopita.

Utawala wake unaangazia hatua thabiti za adhabu ambazo inaweza  kuichukulia  China  kwa namna ambavyo walilishughulikia janga hilo katika siku za mwanzo kabisa 

Kwa upande wa china wao wanadai taifa hilo linataka kuwachafua kwa sababu limeshindwa kupambana na virusi vya corona kama ambavyo lenyewe limefanikiwa

Toka janga hilo lilipuke katika Mji wa Wuhan mwezi Disemba, virusi vya corona tayari vimeshathibitishwa kuwapata zaidi ya watu milioni 1.2 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 73,000 nchini Marekani pekee.

 

ALICHOKISEMA RAIS DONALD TRUMP?

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu yake Tump amesema: "Tumepatwa na shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kwetu.Shambulio hili ni baya zaidi ya la Bandari ya Pearl. Hili baya zaidi ya la Kituo cha Biashara cha Dunia (9/11). Hatujawahi kupatwa na shambuli kama hili.

"Na halikutakiwa kutokea. Lingeweza kuzuilika kwenye chanzo chake. Lingeweza kuzuiliwa na china. Lingeweza kuzuiliwa kwenye chanzo chake, lakini hilo halikufanyika.Alipoulizwa iwapo analiona janga hilo kama shambulio la kivita kutoka Uchina, Trump alijibu kuwa kwa sasa adui wa Marekani ni mlipuko wa virusi na si china

"Ninamchukulia huyu adui asiyeonekana virusi vya corona kama vita,"

Aliongezea kwa kusema. "sipendi kabisa jinsi gani alifika hapa, kwa kuwa kulikuwa na uwezekano wa kuzuia."

 


No comments