Goodluck Gozbert is a Tanzanian gospel artist who write songs and sing.Here is his release IPO SIKU which mean THERE IS MY DAY,an in...
LYRICS
For the lyrics of the song,check out here
Intro:
Ni mbali nimetoka
Tena ni ajabu kuwa hai
Maana ningeshakufaga
Ni mengi nimeona
Tena ya kuvunja moyo
Labda ningeshamwacha Mungu
Bridge:
Kama ni misongo ya mawazo
Magonjwa mama, nimepitia, ninazoea
Maumivu ya kudharauliwa, umasikini
Ni kila siku, ninajipa moyo
Refrain:
Ipo siku yangu tu, Ipo Siku
Ipo siku yangu tu
Nami (Niba niba nibarikiwe)
Nami nibarikiwe (nibarikiwe)
Nibarikiwe (nibarikiwe)
Nami nibarikiwe ( nibarikiwe)
Niba, niba, nibarikiwe
Ingawa kwa sasa wananisema vibaya
Nami sishangai – najua ni ya wanadamu hayo
Ingawa sipati na ni kwa muda mrefu
Siachi kuomba; Mungu si kiziwi
Binadamu wema, ukiwa nacho
Kwa sasa waniepuka sina rafiki wa dhati
(Bridge + Refrain)
Miaka imepita, unaombaga mtoto hupati
Vuta subira maana Yeye hachelewi
Ona biashara imeandamwa mikosi hupati
Usimwache Mungu, waganga watakuponza
Mpo kwa ndoa ila nyumbani amani hakuna
Msimwache Mungu – michepuko sio jibu
Umeugua tumaini la kupona hakuna
Usimtazame mwanadamu siku yako imekaribia
Najua Ayaya (Ipooo) x2
Misuko-suko ya ndoa
Mtoto anakusumbua
Giza likiingia unawaza wapi utalala
Masimango Mashemeji, ati huzai mtoto
Masimango mama wa kambo
Umemchosha nyumbani
Usiwaze usiumie, najua yote yatapita
Siku imekaribia, najua yote yatapita
Nawe ubarikiwe (nibarikiwe)
Ubarikiwe (nibarikiwe)
Nawe ubarikiwe (nibarikiwe)
Uba, Uba, Ubarikiweee
No comments