HISTORIA YA KIM JONG UN KIM ni mtoto wa pili wa Kim Jong-il (1941-2011) na Ko Yong-hui. Kabla ya kuchukua madaraka, Kim alikuwa haone...
KIM ni mtoto wa pili wa Kim Jong-il (1941-2011) na Ko Yong-hui.
Kabla ya kuchukua madaraka, Kim alikuwa haonekani mara kwa mara kwa umma.
Maelezo kama vile mwaka gani alizaliwa, na kama alienda kweli shule nchini Uswisi akitumia
jina la uongo, ni vigumu kuthibitisha.
Tangu mwaka 2009 taarifa zilianza kutokea kuwa Kim
aliteuliwa kumfuata baba yake aliyekuwa mgonjwa, akipewa nafasi katika kamati
ya kijeshi. Nyimbo zilianza kutungwa za kusifu familia ya Kim zikitaja jina la
Kim Jong-Un. Mwaka 2010 alipewa cheo cha jenerali jeshini na kuwa makamu
wa mwenyekiti wa kamati kuu ya kusimamia jeshi
Kim alitangazwa kuwa kiongozi mkuu baada ya mazishi ya
baba yake tarehe 28 Desemba 2011. Vyeo vyake ni Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyakazi wa Korea, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, Mwenyekiti wa Tume ya
Mambo ya Ndani, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Watu wa Korea, na mwanachama wa Kamati
ya Kudumu ya Politburo ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea. Mamo tarehe 9 Machi
2014, Kim Jong-un alichaguliwa bila kupingwa kuingia katika Bunge Kuu la Watu.
Kim ana shahada mbili, moja ya fizikia kutoka Chuo kikuu cha Kim II
Sung na nyigine kama afisa wa Jeshi katika Chuo Kikuu cha Jeshi cha Kim
Il-sung.
Tarehe 12 Desemba 2013, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilitangaza kwamba
kwa sababu ya "udanganyifu," aliamuru mauaji ya mjomba wake Jang
Song-Thaet. Kim Jong-un anaaminika kuwa ndiye aliyeamuru mauaji ya kaka yake wa
kambo, Kim Jong Nam nchini Malaysia mwezi Februari 2017.
source:
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kim_Jong-un
No comments