Marehemu Mchungaji Peter Mitimingi wa Kanisa la Ghala la Chakula cha Uzima kwa kiingereza (Warehouse Christian Centre-WCC) ambay...
Marehemu Mchungaji Peter Mitimingi wa Kanisa la Ghala la Chakula cha Uzima kwa kiingereza (Warehouse Christian Centre-WCC) ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Voice of Hope Ministry (VHM) ambayo ilikuwa ni huduma inayojihusisha na injili vijijini.
Kabla ya hapo alikuwa ni mchungaji msaidizi wa kanisa la TAG-Mwenge.Katika siku za uhai wake alinukuliwa akisema
"Sijatoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa ugomvi kama watu wanavyozusha bali nilikwenda kwa viongozi wa juu wa Kanisa. Nilianza na nyumbani Mwenge TAG ambapo nilikuwa mchungaji msaidizi, nikaenda kwa mchungaji wa wilaya, nikaenda kwa Makamu wa Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dkt. Magnus Mhiche. Wote hawa walinikubali, wakaniombea na kuniwekea mikono tayari kwa kutumika."
Atakumbukwa kwa masomo yake imara ya mahusiano ambayo yalisaidia kujenga ndoa na kuwapa utashi vijana juu ya mahusiano.
CHANZO CHA KIFO CHAKE
Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo Samwel, amethibitisha taarifa za kifo na chanzo chake
“alikuwa anaumwa Sukari ilipanda, ikaanza homa ya mapafu kwasababu alikuwa Arusha akapigwa na mvua kukawa na baridi kali ikamsumbua”
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa,Jina lake libarikiwe!
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa,Jina lake libarikiwe!
No comments