Mauaji ya mtafiti wa masuala ya virusi vya corona kutoka China yaliyotokea Marekani yamesababisha nadharia mbalimbali duaniani kuwa kuna uwe...
Mauaji ya mtafiti wa
masuala ya virusi vya corona kutoka China yaliyotokea Marekani yamesababisha
nadharia mbalimbali duaniani kuwa kuna uwezekano mkubwa nyuma ya pazia kukawa na
sababu nzito iliyojificha kuhusu kifo chake.
Profesa msaidizi Bing Liu mwenye miaka 37 katika Chuo Kikuu cha Tiba
cha Pittsburgh,alikutwa nyumbani kwake huko Marekani siku ya jumamosi akiwa
ameaga dunia.
Watu wake wa karibu wanadai kuwa alikuwa karibu kupata matokeo muhimu ya tafiti kuhusu Covid-19, tukio lililosababisha
kuwepo kwa maoni mitandaoni yanayoeleza kuwa yawezekana profesa Liu aliuawa
lakini polisi wanasema kuwa tokio la kifo cha bwana Liu ni la kujiua.
Chanzo cha kifo cha Professa Liu?
Alikutwa akiwa na majeraha mengi ya risasi kichwani na shingoni
katika eneo la Pittsburgh ambapo ndipo yalipo makazi yake kwa mujibu wa polisi
wa eneo hilo.
Mtu aliyekuwa na silaha alitambulika kuwa na miaka 46, mhandisi wa programu ya kompyuta (software engineer), Hao Gu.
Mamlaka zinasema muuaji naye alijiua baada ya kurudi kwenye gari lake.
Liu na Gu walikuwa wanafahamiana, maafisa
wapelelezi wa mauaji walieleza.
Uchunguzi umebaini kuwa lilikuwa tukio la kuua na kujiua
lililotokana na mgogoro wa muda mrefu wa
masuala ya kimapenzi.
Wamesema ''hakuna
ushahidi'' wa kuhusisha tukio hilo na utafiti wa Liu na mazingira ya sasa
ya changamoto za kiafya.
Professa Liu ni nani?
Katika taarifa yao , watu wake wa karibu wamemwelezea kama mtafiti wa
kipekee ambaye alikuwa ukingoni kufanikisha kupata matokeo muhimu ya
kuelewa maambukizi ya virusi vya corona.
Waliomboleza kifo cha Liu na kuahidi kumalizia utafiti wake
zikiwa ni juhudi za kuenzi ubora wake katika uwanja wa kisanyansi.
Liu, raia wa China alipata shahada yake ya kwanza na shahada
ya uzamivu katika masomo ya sayansi ya kompyuta nchini Singapore kabla ya
kufanya utafiti nchini Marekani.
Aliwahi kuungana na wanabaiolojia wengine kufanya utafiti
kuhusu kinga ya binaadamu, kwa mujibu wa wasifu wake mtandaoni.
Wadau wengi mitandaoni wanalaumu na kudai kuwa kifo hicho kimefichwa nyuma ya wivu wa kimapenzi.
No comments