Shirika la Afa Duniani ( WHO) limeyakataa madai ya rais wa Tanzania John Magufuli kwamba kumekuwa na kasoro katika vifaa vya kupimia vir...
Shirika la Afa Duniani ( WHO) limeyakataa
madai ya rais wa Tanzania John Magufuli kwamba kumekuwa na
kasoro katika vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini humo. Katika taarifa
yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa WHO kwa Afrika Matshidiso Moeti
amesema hawakubaliani na kile alichokisema rais Magufuli. Taarifa hiyo
inatolewa baada ya Jumapili iliyopita rais huyo wa Tanzania kusema vifaa vya
kupima vimekuwa na kasoro, na kubaini kupatikana kwa virusi vya corona katika
papai na mbuzi
Pia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC)
nacho kimesema kwamba vifaa vinavyotumika kupimia virusi vya corona nchini
Tanzania havina shida yoyote. Leo alhamisi, Mkuu wa Afrika CDC Dkt.
John Nkengasong amezungumza na waandishi wa habari kupitia mtandao
katika ofisi yake na amenukuliwa akisema;
"Vipimo ambavyo Tanzania inatumia tunajua kwamba
vinafanyakazi vizuri!"
Kauli hiyo ya Mkuu wa Africa CDC, inapingana na kauli
aliyoitoa rais wa Tanzania ambaye alisema huenda vipimo hivyo vikawa na matatizo.
Kituo hicho cha Africa CDC pamoja na wakfu wa Jack
Ma, Shirika la msaada la bilionea wa China, lilisambaza vifaa hivyo, Nkengasong amesema
na kuongeza kwamba vilidhinishwa na wanachojua ni kwamba vinafanya vizuri.
Kituo hicho kiko chini ya Umoja wa Afrika kina majukumu
ya kuratibu mapambano dhidi ya mlipuko wa mangonjwa barani Afrika.
source:BBCswahili and DW swahili
No comments